Hii ni Sober house ya kwanza kuanzishwa Tanzania bara mwaka 2012,na ilianza na waraibu 15 tu,na sasa imesaidia waraibu zaidi ya 3000,na huduma tunazotoa ni tiba kwa waraibu wa pombe,bangi,heroin,cocaine,tramadol,na dawa nyingine za kulevya.


Katika Pilimisanah Foundation Sober House, tunatoa huduma za kina na za kitaalamu kwa ajili ya matibabu ya uraibu na afya ya akili. Kila mteja hupokea huduma kulingana na mahitaji yake binafsi, kwa lengo la kuhakikisha mabadiliko ya kweli, ya kudumu na yenye maana. Huduma zetu ni pamoja na:
Ushauri Nasaha
(Counseling)
Tiba Tambuzi ya Tabia
(CBT – Cognitive Behavioral Therapy)
Afya ya Akili
(Mental Health Services)
Mpango wa Hatua 12
(12 Step Program – Narcotics Anonymous)
Tiba ya Kijamii
(Social Therapy)
Tiba ya Familia
(Family Therapy)
Ujuzi wa Maisha
(Life Skills Training)
Tunatoa ushauri nasaha wa mtu mmoja mmoja, wa kikundi, na wa ndoa au familia, kwa ajili ya kusaidia waraibu kuelewa hali yao na kupata mwongozo wa kihisia na kisaikolojia katika safari ya kupona.
Tiba hii husaidia mteja kubaini na kubadilisha mitazamo, fikra potofu, na tabia hatarishi zinazochochea uraibu.
Tunatambua kuwa changamoto nyingi za uraibu huambatana na matatizo ya afya ya akili. Tunatoa huduma za tathmini, ushauri na ufuatiliaji wa afya ya akili kwa mteja.
Tunatumia mfumo wa kimataifa wa hatua 12 uliothibitishwa kusaidia waraibu kukubali hali yao, kuachana na dawa za kulevya, na kuishi maisha mapya ya uwajibikaji, maadili, na matumaini.
Kupitia shughuli za kijamii, michezo, kazi za pamoja na mijadala ya vikundi, tunawasaidia waraibu kujenga upya mahusiano, mawasiliano, na hali ya kujiamini katika jamii.
Uraibu huathiri familia nzima. Tunahusisha familia katika mchakato wa uponyaji kwa kupitia vikao vya pamoja, elimu ya uraibu, na usuluhishi wa migogoro ya kifamilia.
Tunawafundisha waraibu stadi muhimu za maisha kama vile usimamizi wa muda, nidhamu ya kifedha, mawasiliano, kufanya maamuzi bora, na maandalizi ya maisha baada ya tiba (re-integration).
Tunaamini kuwa kwa kutumia njia hizi za kitaalamu, kila mtu ana nafasi ya kupona, kurejea katika jamii, na kuanza upya maisha yenye matumaini.



Katika safari ya kupona kutoka utegemezi wa madawa ya kulevya, changamoto si tu kuacha matumizi, bali pia kushughulika na madhara ya kiafya yanayoweza kujitokeza baada ya kuacha. Baadhi ya wagonjwa hukabiliana na mshtuko, mabadiliko ya hisia, na maumivu...
Soma zaidiSoma makala hii kufahamu tofauti kati ya detox na rehab, hatua mbili muhimu katika tiba ya uraibu nchini Tanzania....
Soma zaidiJe, Dopamine ni Nini? Huenda umewahi kusikia jina dopamine likitajwa kama "kemikali ya raha" inayohusishwa na tabia za uraibu. Watu wengi hutumia maneno kama “dopamine rush” kueleza msisimko wa ghafla wanaoupata wanapofanya jambo linalowapa raha iwe ni kununua...
Soma zaidiGoogle review